Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuwatazama Yanga vs Vital'O buku 5 tu

Yanga Kikosi At 15 Kikosi cha Yanga

Mon, 19 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa marudiano kati ya Young Africans dhidi ya Vital’O Jumamosi ijayo, viingilio vimetajwa katika madaraja manne.

Kiingilio cha juu ni Tsh 30,000 katika Jukwaa la VIP A, huku kile cha chini kabisa Jukwaa la Mzunguko ikiwa ni Sh 5,000.

Mbali na hivyo, katika mchezo huo ambao tutakuwa wenyeji, Jukwaa la VIP B ni Tsh 20,000 na VIP C Tsh 10,000.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Ikumbukwe kwamba, katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam tukiwa wageni wa Vital’O, tulishinda magoli 4-0 yaliyofungwa na Prince Dube, Clatous Chama, Clement Mzize na Stephane Aziz Ki

Chanzo: www.tanzaniaweb.live