Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuwaona Yanga vs Mamelodi ni bure kwa Mkapa

Mashabiki Yanga Mil 130 Yanga vs Mamelodi ni bure kwa Mkapa

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Yanga SC, Hersi Said pamoja na Kamati yake ya Utendaji wamekubaliana kuwa mechi yao dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini siku ya Jumamosi ya March 30, 2024 itakuwa bure sehemu za mzunguko.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC Ally Kamwe akieleza kuwa wameamua hivyo kwa kuzingatia kuwa mechi inachezwa usiku saa 3:00 hivyo wanawapunguzia Mashabiki gharama.

Yanga wametangaza gharama zao za tiketi zitakuwa VIP A Tsh 30,000, VIP B Tsh 20,000 na VIP C Tsh 10,000.

“Tunafahamu mechi ni usiku sana na tumewafikiria mashabiki na wanachama wetu baada ya mechi muda utakuwa umeenda sana na watatumia gharama nyingi za usafiri wakati wa kurudi nyumbani.

“Viongozi wa Yanga wanegkuwa na tamaa tamaa, watu wa kuchungulia fursa hii mechi wangesema wanapiga pesa, wangeweka viingilio vikubwa tungetafutana hapa.

“Lakini kwa vile na wao wanatambua maslahi ya Taifa, uwepo wa mashabiki pale Uwanjani utaongeza hamasa kwa wachezaji wetu, wakaamua kuachana na maslahi ya fedha na kuchagua mpira ushinde ili watu wengi waje kuishabikia Yanga.

“Sisi kama viongozi chini ya Rais Eng. Hersi Said tumeamua mechi hii katika jukwa la Mzunguko ambalo watu wengi hukaa, mashabiki wote wataingia bure.

“Thamani ya kuiona Yanga na Mamelodi ni kubwa. Kiasi cha fedha ambacho ungelipia tiketi ya mzunguko basi utatumia kama nauli ya usafiri wa kukufikisha uwanjani na baada ya mchezo wetu uweze kurudi nyumbani salama.

“Tunawaomba ambao mtasafiri kutoka maeneo mbalimbali muwahi, mageti yatafunguliwa mapema sana, tuje tuipe sapoti timu yetu," Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: