Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuwaona Yanga na Al Ahly buku tano tu

Mashabiki Yanga Shangwe Kuwaona Yanga na Al Ahly buku tano tu

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viingilio vya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Al Ahly, vimewekwa hadharani huku vikigawanywa kwenye makundi sita.

Kugawanywa kwa viingilio hivyo katika makundi sita, ni kutoa fursa kwa kila mpenda soka hasa mashabiki wa Yanga SC kufika uwanjani kuisapoti timu yao.

Kiingilio cha juu kabisa, ni Tsh 300,000 kwa tiketi ya Royal ambayo ndani yake itakuwa na huduma za V.I.P, usafiri wa kwenda uwanjani na kurudi, jezi moja ya kimataifa 2023-2024 na huduma za vyakula na vinywaji.

Kwa upande wa viingilio vingine, Jukwaa la Mzunguko ni Tsh 5,000, Jukwaa la Orange Tsh 10,000, V.I.P C Tsh 20,000, V.I.P B Tsh 30,000 na V.I.P A Tsh 50,000.

Mchezo huo wa Kundi D, unatarajiwa kuchezwa Jumamosi ya wiki hii Desemba 2, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, Yanga imetangaza kwamba, endapo utanunua tiketi kwa kadi hai ya uanachama Makao Makuu Jangwani, utapata punguzo la asilimia 50.

Ili kupata tiketi ya Royal, wasiliana nao kupitia namba 0743347312.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live