Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuwaheshimu Yanga ni nusu ya kuwakabili

Yanga Tizi Kali Kuwaheshimu Yanga ni nusu ya kuwakabili

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga V/s KMC FC ni mechi nzuri kuitazama, ukiangalia namna ambavyo KMC wameanza Ligi kuna baadhi ya vitu vimeonekana kwenye mchezo uliopita [Namungo FC 1-1 KMC FC] vinaonesha ni vitu chanya na vinaweza kuwasaidia kwenye mchezo wa leo kama wataingia kwa kuiheshimu Yanga.

Kama KMC wataiheshimu Yanga kwa ubora na wachezaji ilionao maana yake tayari ni nusu ya kuikabili, kwa sababu watakuwa wametambua aina ya mpinzani wanaekutananae ana kitu gani.

Wakiingia kwa ule msemo wao wapo 11 na sisi tupo 11, tayari watajiweka kwenye wakati mgumu kwakuwa watakuwa hawajatambua ubora wa wachezaji na timu wanayochezanayo.

Yanga ni bingwa wa Ligi Kuu kwa misimu miwili iliyopita na leo wanaanza kampeni ya kutetea ubingwa huo kwa mchezo wao wa kwanza wa Ligi msimu huu wa 2023|24.

Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa KMC, ililazimika kuche play offs ili kujihakikishia kubaki kwenye Ligi bila shaka wamejifunza walipokosea msimu uliopita na wamerekebisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live