Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Kutakuwa na tofauti ya pointi 25 kati ya Man Utd na Man City'

'Kutakuwa Na Tofauti Ya Pointi 25 Kati Ya Man Utd Na Man City'.png 'Kutakuwa na tofauti ya pointi 25 kati ya Man Utd na Man City'

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Meneja wa Kidderminster Phil Brown anaamini kuwa Manchester City bado itamaliza pointi 25 bora zaidi kuliko wapinzani wao Manchester United kwenye Ligi ya Premia msimu huu, licha ya Erik ten Hag kununua wachezaji wapya katika soko la usajili ili kuimarisha kikosi chake.

Mabingwa wa Kombe la FA United walimaliza katika nafasi ya nane kwenye ligi msimu uliopita, pointi 31 nyuma ya mabingwa City.

"Manchester United kwa sasa, sio klabu ambayo wachezaji wanaingia na kuanza kujituma sio kulala na kuchukua muda muda," Brown aliambia Football Daily.

"Ulikuwa msimu mgumu sana kwa [Manchester] United, lakini walimaliza kifua mbele kidogo kwa [kushinda Kombe la FA], unaweza kusema.

"Sikuona mechi ya kombe la Ngao ya Jamii Jumamosi, lakini bado nasema kutakuwa na tofauti ya pointi 25 kati ya Manchester United na Manchester City msimu ujao."

Chanzo: Bbc