Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kurudi Simba bora nikauze ndimu - Victor Costa

Costa Pic Victor Costa

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huyu ni Kiungo bora sana ambaye alitikisa Tanzania Kwenye Uwanja wa Soka, kipaji ambacho kilitambulishwa Kwenye Soka la Ushindani na Neidor Santos pale Simba baada ya Victor Costa na wenzake kujivunja.

Nyota huyu alipata nafasi ya kucheza sambamba na Kelvin Yondani na Henry Joseph. Baada ya kupata nafasi nyota huyu akafanya kweli mwisho wa siku akawa mchezaji mkubwa Kwenye medani ya Soka la Bongo.

Nguli huyu alipewa jina la Mapafu ya Mbwa Kwa sababu ya ubora wake wa kutawala eneo la kati pia akiwa na uwezo mkubwa wa kucheza kama mlinzi wa Kati na akakupa faida .

Baada ya Kutamba Msimbazi, YANGA wakambeba Ndipo akatoa kauli nzito kwamba

"KURUDI SIMBA BORA NIKAUZE NDIMU"

Haya ni maneno ambayo wakongwe wa enzi zangu hawasahau kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live