Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kurt Zouma ahukumiwa kwa Kosa la kumpiga Paka

Kourt Zouma Adhabu Beki wa West Ham, Kourt Zouma

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa West Ham United Kurt Zouma ameagizwa kufanya kazi za kijamii kwa saa 180 baada ya kukiri kosa la kumpiga teke na kofi paka wake.

Zouma mwenye umri wa miaka 27 pia amepigwa marufuku kufuga paka kwa kipindi cha miaka mitano.

Alikiri makosa mawili chini ya Sheria ya Ustawi wa Wanyama wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake katika Mahakama ya Thames mwezi Mei.

"Paka alikuangalia wewe ili umtimizie mahitaji yake. Tarehe hiyo ya Februari hukutoa mahitaji yake. Lazima ufahamu kwamba wengine wanakutazama na vijana wengi wanatamani kukuiga."

Kaka yake Zouma, Yoan, anayechezea klabu ya Dagenham & Redbridge, aliamriwa kutekeleza saa 140 za huduma ya Kijamii katika kesi hiyo ya dakika 15 baada ya Yoan kukiri shtaka moja la kusaidia na kumshauri kaka yake mkubwa kutenda kosa.

"Nyinyi wawili mlishiriki katika kitendo hiki cha aibu na cha kulaumiwa kwa paka huyu," hakimu wa wilaya Susan Holdham alisema.

Yoan, 24, alirekodi tukio hilo nyumbani kwa kaka yake mkubwa na kulichapisha kwenye Snapchat na emoji za 'vicheko' mnamo 6 Februari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live