Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kura Ujerumani zamkataa Havertz Euro 2024

Kai Havertz Eurooo Kai Havertz

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa timu ya taifa ya Ujerumani wanamtaka Kai Havertz apigwe chini kwenye kikosi kinachoshiriki fainali za Euro 2024.

Straika huyo ameazishwa kwenye mechi zote tatu za makundi ilizocheza Ujerumani kwenye fainali hizo chini ya kocha Julian Nagelsmann.

Na kwenye mechi hizo, amefunga bao moja, mkwaju wa penalti dhidi ya Scotland, lakini alipoteza nafasi nyingi sana za kufunga kwenye mechi dhidi ya Hungary na Uswisi.

Matokeo yake yamefanya mashabiki kumtaka aondoshwe kweye kikosi cha Ujerumani cha mastaa watakaoanza katika mchezo wao ujao wa hatua ya 16 bora kwenye fainali hizo zinazofanyika kwenye ardhi ya kwao.

Kura 138,000 za mashabiki wa soka wa Ujerumani, asilimia 90 zilitaka staa huyo wa Arsenal aondoshwe kwenye kikosi kinachoanza Ujerumani.

Na mashabiki hao, wengi wakimpa nafasi straika Niclas Fullkrug kumbadili Havertz, kwa sababu ndiye namba 9 wa asili.

Fullkrug, 31, alifunga pia kwenye ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Scotland na alifunga bao la dakika za mwisho la kusawazisha dhidi ya Uswisi.

Amekuwa na rekodi tamu kwenye kikosi cha Ujerumani akifunga mabao 13 katika mechi 19 huku kocha Nagelsmann akikiri kwamba anaweza kushawishika kuanza naye kwenye mchezo ujao.

Kocha huyo wa Ujerumani alisema: “Fulle ana nafasi ya kuanza, lakini Kai naye ana nafasi pia. Kai alipata nafasi tatu nzuri na inachukiza ameshindwa kutumia walau hata mbili tu. Unaweza kuwa na mjadala juu ya hilo. Kuna mtu unaweza kuanza naye benchi na anakwenda kufanya vizuri, anakushangaza kama yule aliyefunga akitokea benchini.”

Chanzo: Mwanaspoti