Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kupata mshambuliaji mzuri dirisha dogo ni ngumu - Gamondi

Gamondi X Konkoni Kocha Gamondi.

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa ni ngumu kupata mshambuliaji mzuri kwenye dirisha dogo la usajili kwani wachezaji wengi wanakuwa bado wana mikataba.

Gamondi amesema hayo wakati timu yake ikihaha kusaka mshambuliaji atakayeziba nafasi ya Fiston Mayele baada ya kennedy Musonda na Hafiz Konkoni kushindwa kufikia matarajio ya Wananchi wa Jangwani.

"Tunatafuta mshambuliaji lakini kwenye dirisha dogo ni ngumu kupata mchezaji kwa sababu wachezaji wengi wazuri wapo kwenye mikataba na timu zao na klabu hawawezi kuwaachia kirahisi wachezaji wao lakini watu wanapaswa kujua kumpata mshambuliaji kuna vitu viwili.

"Mosi ni kujua mchezaji gani anapaswa kusajiliwa lakini pili ni kiwango gani cha fedha tunacho kwa ajili ya kupata mchezaji husika," amesema Kocha Miguel Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live