Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kununuliwa kwa mkwanja mrefu kumempa hamasa Jude Bellingham

Jude Bellingham Real Madrid Kununuliwa kwa mkwanja mrefu kumempa hamasa Jude Bellingham

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jana baada ya mechi ya England V/s Italy nilifatilia interview ya kinda wa Real Madrid na England, Jude Bellingham ambaye kwa sasa yupo kwenye kiwango bora sana!

Bellingham anasema watu wengi wanazungumzia kiwango chake kuwa juu kwa sasa, akasema hakuna kitu ambacho kimemuongezea uwezo kama kujiunga na Real Madrid.

Akataja baadhi ya vitu ambavyo vinachochea yeye kuwa katika kiwango bora tangu amejiunga na Real Madrid akitokea Borussia Dortmund.

Ada ya uhamisho, anasema mchezaji akinunuliwa kwa gharama kubwa inakupa deni kichwani. Kila mechi unayocheza sio tu unalazimika kufunga au kutoa assist bali unapaswa kucheza kwa kiwango ambacho kitaisaidia timu kupata ushindi.

Kwa hiyo mchezaji kununuliwa kwa gharama kubwa haikufanyi ubweteke, inakuongezea hamasa na kukupa mzigo mkubwa ambao wengine umewashinda.

Real Madrid ni klabu kubwa yenye wachezaji wenye viwango vikubwa, kwa hiyo kuwa sehemu ya klabu ya aina hiyo inayokukutanisha na wachezaji wakubwa unafanyanao mazoezi, unakutananao dressing room na kuchezanao, inakusaidia kuongeza kiwango chako.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live