Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kundi la pili la wachezaji Simba sasa kuondoka nchini Julai 17

Kikosi Simba 1140x640 Kundi la pili la wachezaji Simba sasa kuondoka nchini Julai 17

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la pili la wachezaji wa Simba SC linatarajia kuondoka nchini Julai 17, 2023 kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi badala ya Julai 15 iliyotangazwa awali.

Kundi la kwanza la wachezaji 18 na benchi la ufundi liliondoka Julai 10, 2023 kuelekea Uturuki ambapo wakiwa nchini humo, wanatarajia kucheza mechi tatu za kirafiki kabla ya kurejea Agosti Mosi, 2023.

Wachezaji hao waliondoka ni:

Makipa:

Ally Salim, Ahmed Feruz

Walinzi:

Shomari Kapombe, Henock Inonga, Kennedy Juma, Israel Mwenda, David Kameta na Mohammed Hussein

Viungo:

Sadio Kanoute, Nassor Kapama, Kibu Denis, Jimmyson Mwanuke, Peter Banda, Saidi Ntibazonkiza na Mzamiru Yassin.

Washambuliaji:

Moses Phiri, John Bocco na Mohamed Mussa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live