Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kundi D Mapinduzi Cup pasua kichwa

Namungo Mapinduzi Kundi D Mapinduzi Cup pasua kichwa

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi D lililo na timu ya Aigle Noir kutoka Burundi, Namungo Tanzania Bara na Chipukizi limeonekana kuwa gumu kutokana hadi sasa kinara wa kundi hilo kuwa na pointi mbili.

Chipukizi ndio inaongoza kundi baada ya kuanza na sare ya bao 1-1 dhidi ya Aigle Noir na leo imeambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo sasa inasubiri matokeo ya mchezo uliobaki kuamua nani atatinga hatua ya nusu fainali.

Ijumaa hii Namungo na Chipukizi watakutana mchezo utakaoamua timu itakayo tinga hatua ya nusu fainali ambayo hadi sasa ni Simba tu ambayo imeondolewa.

Huku timu nyingine zote zikisubiri mechi ya mwisho iweze kuamua nafasi yao ya kutinga hatua ya nusu fainali na mechi ya mwisho itachezwa Januari 8 mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live