Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Zanzibar (ZLB) imeyafuta matokeo ya Mchezo wa Ligi Kuu kati ya Kundemba dhidi Zimamoto mchezo ulioshindwa kuendelea ambao ulikuwa ukingoni kumalizika na matokeo yakiwa 2-2.
Mchezo huo uliochezwa Novemba 22, 2023 kwenye Uwanja wa Mao Zedong na kushindwa kumalizika kwa wakati ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ZLB Zimamoto wamepewa alama tatu na Magoli mawili huku Kundemba FC wakitozwa Faini ya Sh Million Saba na Laki mbili (7,200,000).
Mchanganuo wa Faini hiyo ya Kundemba FC:-
Milioni 5,000,000 Kosa la Mshabiki wao kumpiga Muamuzi.
Million 2,000,000 kosa la kusababisha ghasia na kupelekea Mchezo kushindwa kumalizika.
Laki 200,000 kosa la Wachezaji wake kupewa kadi tano za adhabu.
Kamati imemfungia Mshabiki Abdul Rahman [Vieri] wa Kundemba kutojihusisha na Mpira wa Miguu kwa kipindi cha Miaka miwili ambapo mshabiki huyo anahusika kuwa chanzo cha vurugu zilizopelekea mchezo huo kushindwa kumalizika.