Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuna watu watachukua miaka 50 kufika tulipo - Ahmed

Ahmed Ally Semaji La Simba.jpeg Kuna watu watachukua miaka 50 kufika tulipo - Ahmed

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Semaji la CAF, Ahmed Ally ametamba kuwa, kwa mafanikio waliyoopo, kuna baadhi ya timu zitachukua takriban miaka 50 kufika mahala walipo.

Ahmed ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2023 wakati alipokuwa akifanya hamasa ya kuelekea mchezo wao wa African Footbal League dhidi ya Al Ahly utakaochezwa Oktoba 20, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

"Itawachukua wengine si chini ya miaka 50 kutufikia tulipo na hatujaridhika, tunataka nafasi ya Al Ahly ya ubora barani Afrika kuwa namba moja na tutaichukua. Hakuna kinachoshindikana kwa Mnyama akitaka jambo lake."

"Dhamira yetu sio tu kumfunga Al Ahly, tumeshamfunga sana, safari hii tunataka kumtoa, na wamekuja wakati mbaya, wakati ambao tunataka sifa barani Afrika. Hatutamuacha salama."

"Mpango wa kumtoa Al Ahly unaanza na wewe Mwanasimba kuja Kwa Mkapa. Siku hiyo funga shughuli zako mapema, wa kuswali tutasali pale karibu na uwanja baada ya hapo tutaingia ndani kuenjoy, kuna burudani za kumwagika."- Ahmed Ally. #AFL #WenyeNchi #NguvuMoja 1h

Chanzo: www.tanzaniaweb.live