Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuna timu ishajijua inaishia robo - Mchambuzi

Ahmed Kamwez Kuna timu ishajijua inaishia robo - Mchambuzi

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia runinga ya TV3, Boiboi Mkali, amesema kuwa timu moja ya Tanzania tayari imeshajua kuwa itaishia robo fainali ya CAFCL na haitaweza kutoboa kwenda nusu fainali.

Mkali amesema kuwa, ndiyo maana timu hiyo imeanza kuzungumzia mwenzake badala ya kuzungumzia mechi yake.

Itakumbukwa kuwa Tanzania imeingiza timu mbili kwenye hatua ya robo fainali ambazo ni Simba atakayecheza na Al Ahly mnamo machi 29, na Yanga ambaye atacheza na Mamelodi Sundowns, Machi 30.

Hivi karibuni Meneja habari wa Simba, Ahmed Ally aliwaponda Yanga kwa kutangaza kiingilio bure kwenye mechi yao huku Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe akimtaka azungumzie mechi yao na Ahly na si kuwazungumzia Wananchi na Masandawana.

"Hali ilivyo mpaka Sasa Kuna timu ishakubali kuwa wao wameshatoka hivyo wanaenda tu kukamirisha ratiba lakini ndani ya mioyo yao wanajua kabisa kuwa wametoka na ndo maana wapo busy sana kuizungumzia mechi ya wenzao kuliko mechi yao kwakuwa wao wanajua kuwa washatoka," amesema Boiboi Mkali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live