Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuna nini Mo Dewji na Simba?

Mangungu Mo Dewji Mo Dewji na Mangungu

Tue, 21 May 2024 Chanzo: Farhan Kihamu

Leo nimeamka nikarejea Interview ya MO Dewji kuhusu mabadiliko ya kimfumo ndani ya Simba, nimejisikia aibu kama Mwandishi wa Habari yani tangu aseme kuwa kuna Watu wanakwamisha mchakato wa mabadiliko ndani ya Simba, mpaka leo hatujafanya uchunguzi kujua ni nani anakwamisha kwa maslahi gani?

Bado tena nimejisikia aibu mpaka leo hatujaenda in details kufahamu palipokuwa panavuja pamezibwa? Mchakato umefikia wapi? Na lini tutegemee mchakato kusogea mbele? Tulianza kabla ya Yanga na Yanga wanaelekea kumaliza mchakato sisi bado tupo pale pale.

Timu ipo kwenye nyakati mbaya sana haifanyi vizuri, ukiingia kwenye mambo ya kimuundo hatufanyi vizuri, tiba ni nini? Aendelee kulaumiwa MO ambaye pia analaumu mchakato kukwamishwa? Mashabiki na Wanachama ni rahisi kusema MO hatoi hela tuachie timu lakini ni ngumu kuhoji mchakato unapofia?

Ni aibu iliyoje? Timu haina Wanachama wapya kwa miaka sasa, ni aibu iliyoje timu kubwa kama Simba inayojivunia Mashabiki wengi na haina Wanachama wengi? Matokeo yake mzigo unamwelemea Tajiri na mbele hakuna mwanga, Tajiri ameshaongea amemaliza kuwa mchakato unakwama, unakwamia wapi na kwanini? Hatuelewi.

Bila Wanachama wapya, timu maana yake haina mawazo mapya! Wenye mawazo mapya hawana sifa za kugombea ama kuingia kwenye Uongozi, maana yake timu ipo kama kisiwa inaelea! Mwisho wa siku? Tiba ya kwanza ni mabadiliko ya kimfumo, ile 51% ni mfu inapaswa kuwa hai.

Chanzo: Farhan Kihamu