Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuna kitu Ronaldo ametuficha

Ronaldo And Son Kuna kitu Ronaldo ametuficha

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja kati ya siri kubwa ambayo imefichwa na Cristiano Ronaldo ni kuhusiana na ukweli kuhusu mtoto wake anayefahamika kama Cristiano Ronaldo Jr, mpaka leo watu wengi hajapata kufahamu ni nani haswa Mama mzazi wa Cristiano Ronaldo Jr.

Zimebaki nadharia tu ambazo baadhi ya watu wanasema ni mtoto ambaye Cristiano Ronaldo amempata kwa njia ya maabara, lakini nadharia kubwa zaidi ni ile ambayo inasema Cristiano Ronaldo amempata mtoto huyu baada ya kuwapo nchini Marekani kwenye mapumziko yake.

Akiwa huko alikutana na muhudumu aliyempenda na baada ya yote, Cristiano Ronaldo alihisi asingeweza kuonana nae tena, lakini baada ya miezi Cristiano Ronaldo alishangaa kupokea taarifa kutoka kwa mwanamke huyo kwamba yuko ujauzito,

Kwenye moja ya mahojiano Cristiano Ronaldo aliwahi kunukuliwa akisema; "Siwezi kumdanganya Cristiano Ronaldo Jr kwani anapaswa kufahamu ukweli, lakini siwezi kumwambia kwa sababu watu wanatamani kufahamu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live