Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuna kina Majogoro wengi wanapoteza muda Ligi Kuu Bara

Majogoro Sauzi Baraka Gamba Majogoro

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Jumanne wiki iliyopita Baraka Majogoro alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika pambano la Ligi Kuu ya Afrika Kusini kati ya timu yake Chippa United dhidi ya Supersport. Ni miongoni mwa hatua kubwa ambazo zimechelewa.

Nilikimbiliia Wikipedia kuangalia umri wake. Ana miaka 27. Anachofanya inawezekana kitawashangaza wengi lakini binafsi sishangazwi na anachofanya. Ni kitu cha kawaida ambacho kilipaswa kufanywa na kina Majogoro wengi wanaocheza soka Tanzania.

Niliwahi kumuona na kumchunguza Baraka kabla hajaondoka. Alikuwa kiungo hasa. Umiliki wa mpira, upigaji pasi, ukokotaji wa mpira na mengineyo. Kuna viungo wengi wenye ubora wake wapo nchini ingawa walipaswa kuzijaza Ligi mbalimbali za Afrika na Ulaya.

Kama wanamshangaa sana Baraka kiasi wanampa uchezaji bora wa mechi nadhani wangemshangaa zaidi Sure Boy, wangemshangaa zaidi Jonas Mkude, wangemshangaa zaidi Ibrahim Ajibu, wangemshangaa pia Fei Toto. Wangewashangaa wachezaji wetu wengi ambao wanamalizia soka nchini.

Mwingine ambaye amechukua hatua kubwa ya kwenda kucheza nje ni Abdulrazak Hamza anayekipiga katika klabu ya SuperSport. Ni beki imara ambaye ameondoka nchini kimya kimya na sasa anacheza pale Afrika Kusini.

Wenzetu wa nchi za SADC wamejaza wachezaji Afrika Kusini na nchi nyingine ambazo zinalipa vizuri katika soka. Kuna wachezaji wengi wa aina ya Majogoro ambao wanapatikana nchini na wangeweza kuimbwa au kushangaza katika nchi za watu.

Tatizo? Kuna suala la ‘connection’. Wachezaji wetu bado hawafahamiki kwa mawakala wengi ambao wanapeleka wachezaji katika nchi mbalimbali. Lakini jaribu kufikiria tu kama Majogoro angekwenda Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 22. Angewashangaza zaidi.

Lakini pia kuna suala la wachezaji wenyewe kutotamani kucheza nje. Hii inatokea zaidi pale wanapogusa Simba na Yanga. Majogoro anaingia katika orodha ya wachezaji wengi ninaowafahamu ambao wamekwenda kucheza nje bila ya kugusa Simba na Yanga.

Tuna wachezaji wenye ubora ambao wanacheza timu nyingine za kawaida lakini ndoto zao ni kucheza Simba na Yanga. Wakigusa tu Simba na Yanga basi wanaingiwa na utamu ambao inakuwa ni vigumu kuondoka.

Kama sio wao kutotamani kuondoka basi hata klabu zenyewe zimekuwa zikiwabania na kuwabembeleza wasiondoke. Wale ambao hawajaonja raha hizi ndio ambao wanaamua kuondoka na kwenda kujaribu. Orodha ni ndefu.

Nizar Khalfan, Thomas Ulimwengu, Eliuter Mpepo, George Mpole, Novatus Dismas ni miongoni mwa mastaa wengine ambao walifanikiwa kwenda nje kabla ya kugusa Simba na Yanga. Huyu Majogoro anaweza kuwa kama Zawadi Mauya lakini ni ngumu kwa Zawadi kwenda nje.

Kiungo kama Cleophas Mkandara angeweza kucheza nje kwa mafanikio tu lakini nadhani ndoto yake ilikuwa kucheza Simba au Yanga. Baadaye alitimkia Azam FC akitokea Dodoma Jiji lakini mambo hayakwenda sawa kwa sababu alikuwa amerundikiwa viungo.

Leo bado yupo nchini na huenda akawa amevunjika moyo kwa sababu hakucheza Azam kwa mafanikio. Labda angeambiwa stori ya Nonda Shaaban Papii ambaye alikuwa anawekwa benchi pale Yanga lakini baadaye akaibukia kuwa mchezaji mkubwa katika klabu za Ulaya.

Nawafahamu wachezaji wengi ambao wana uwezo wa kucheza katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini kwa mafanikio. Ni moja kati ya Ligi ambazo tulipaswa kuzionea.

Wakati huu kukiwa kuna mafuriko ya wachezaji wa kigeni katika soka letu, bado tunaacha wazawa wengi walio bora ambao wangeweza kwenda kucheza katika klabu za nje. Mpira hauna fomula na ndio maana Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu waliwahi kutamba Congo halafu Fiston Mayele anatamba Tanzania.

Tatizo letu kubwa ni kwamba hata wachezaji walio bora katika klabu nyingine wanasikilizia tu kwamba siku moja wanaweza kuchukuliwa na Simba na Yanga. Kama Majogoro anatamba Afrika Kusini, itamshinda nini Yusuph Kagoma wa Singida Big Stars kucheza Afrika Kusini? Mmoja kati ya viungo maridadi wazawa kwa sasa. Na yeye usikute anasubiri kuchukuliwa na Simba na Yanga.

Wachezaji waamke. Wasisubiri kucheza Simba na Yanga tu. wanaweza kufanya utaratibu mwingine. Sawa wanajitahidi kwa sasa. Kitendo cha kuita wachezaji 13 wanaocheza nje katika timu ya taifa sio kitu kidogo. Lakini kwa idadi ya Watanzania milioni 64 kwa mujibu wa sensa, idadi hiyo ni kidogo. Inapaswa wafanye zaidi.

Nchi za kisoka kama Brazil na Nigeria ambazo zina idadi kubwa ya watu huwa zinanufaika na wachezaji wake kutoka zaidi kwa sababu mkate wa nyumbani hautoshi. Nchi kama India na China sio nchi za kisoka kwahiyo idadi yao haiwasaidii katika kutoa wachezaji wengi.

Tanzania ilipaswa kuzifunika nchi nyingi za jirani na kwingineko kwa sababu ya idadi yake ya watu lakini pia watu wanacheza mpira. Hiki ndicho kitu ambacho kilimshangaza Jay Jay Okocha alipokuwapo nchini wiki iliyopita.

Wachezaji wetu waamke. Kitu kama hiki alichofanya Majogoro kinapaswa kuwa kitu cha kawaida tu kwa wachezaji wetu. Wala sio maajabu. Tatizo letu kubwa ni kusubiri kucheza Simba na Yanga. Inaturudisha nyuma.

Anko Mrisho Ngassa alikwenda Afrika Kusini huku miguu ikiwa imemsaliti lakini kama angeenda na ule moto wake sasa hivi angekuwa anamaliza mpira huku akiwa na kipato kikubwa cha pesa. Ni kosa ambalo hatalisema hadharani lakini moyo wake utakuwa unajua hivyo.

JUMANNE wiki iliyopita Baraka Majogoro alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika pambano la Ligi Kuu ya Afrika Kusini kati ya timu yake Chippa United dhidi ya Supersport. Ni miongoni mwa hatua kubwa ambazo zimechelewa.

Chanzo: Mwanaspoti