Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuna kilichopo nyuma ya Pazia usajili wa Ronaldo kwenda Al-Nassr?

Cristiano Ronaldo Al Nassr Saudia Cristiano Ronaldo

Fri, 13 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu mpya ya Cristiano Ronaldo ya Al-Nassr imekanusha ripoti kwamba mkataba wake unajumuisha makubaliano ya kuunga mkono ombi la pamoja la Saudi Arabia kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2030.

Ronaldo, 37, alijiunga na Al-Nassr mwezi uliopita baada ya kuondoka Manchester United kwa makubaliano mnamo Novemba baada ya mahojiano yake na Piers Morgan.

Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or aliweka bayana juu ya mkataba mkubwa wenye thamani ya paundi milioni 175 kwa mwaka na Al-Nassr, ambao kwa sasa wanashikilia usukani wa Ligi Kuu ya Saudia.

Walakini, ripoti kutoka Hispania mwishoni mwa Disemba zilidai Ronaldo pia anatazamiwa kuwa balozi wa ombi la Saudia kuandaa Kombe la Dunia la 2030 kwa sababu ya kifungu katika mkataba wake wa Al-Nassr.

Hata hivyo Al-Nassr wamekanusha kuwa ndivyo ilivyo, huku klabu hiyo mpya ya Ronaldo ikienda kwenye Twitter kutupilia mbali mapendekezo kwamba mkataba wake una kipengele cha kuunga mkono zabuni za Kombe la Dunia.

Katika taarifa fupi ya Jumanne usiku, waliandika: ‘Al Nassr FC ingependa kufafanua kwamba kinyume na taarifa za habari, mkataba wa Cristiano Ronaldo na Al Nassr haujumuishi ahadi za zabuni zozote za Kombe la Dunia. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!.

“Lengo lake kuu ni kwa Al Nassr na kufanya kazi na wachezaji wenzake kusaidia klabu kupata mafanikio.”

Wakati Al-Nassr wakisisitiza kuwa Ronaldo hahusiki, Messi tayari ametambulishwa kuwa balozi wa Saudia.

Ronaldo bado hajacheza mechi yake ya kwanza na Al-Nassr huku akiendelea kutumikia adhabu yake ya kutocheza mechi mbili duniani kote kutoka kwa FA kwa kosa la kuvunja simu ya shabiki wa Everton mwaka jana.

Safari yake ya kwanza katika klabu hiyo inaweza kumkabili Messi, kwani Januari 19 wanaripotiwa kupangwa kukutana na PSG katika mchezo wa kirafiki mjini Riyadh, kwa mujibu wa The Guardian.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live