Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuna Yao alafu kuna Lusajo

Lusajo Mwaikenda Azam FC Lusajo Mwaikenda

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja kati ya Walinzi vijana wenye takwimu bora ndani ya NBC kwa hapa ilipofikia, akiwa ameshacheza Michezo 6 tayari ameshatengeneza nafasi za mabao 2.

Lusajo kiuhalisia ni Mlinzi wa kati ila kutokana na klab yao kukosa Mlinzi wa kulia mwenye

Ubunifu

Utulivu

Umakini wa kila tukio la Uwanjani basi Wakufunzi wengi ndani ya Azam Fc wamembadilisha na sasa anatumika katika nafasi ya Ulinzi wa kulia,

Lusajo ambaye ni, Ana nidhamu kubwa sana ya Mchezo kwa maana kukaba, kushambulia na hata kutengeneza nafasi.

Yao-Ukiachana na Mlinzi wa kulia wa klabu ya Yanga Yao Kouassi ambaye mpaka sasa ana Pasi za magoli 3 na goli la kufunga basi nyuma yake yupo Mnyakyusa wa Dar Lusajo Mwaikenda,

Ni nadra sana kuona akimaliza msimu bila kuwepo kwenye orodha ya walinzi wanaofunga na wanao tengeneza pia nafasi za kufunga,

Pia Lusajo ni bora zaidi ya sasa anapotumika katika nafasi ya Ulinzi wa kati iwe na kusimama na Malickou , Amoah ama Sebo.

Lusajo ni tumaini jipya la Taifa katika nafasi mbili tofauti za Ulinzi yaani Ulinzi wa kulia na hata ulinzi wa kati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live