Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumpata Bellingham mjipange sana

Jude Belligham JJ Jude Bellingham

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kama kuna timu inataka huduma ya kiungo wa Borussia Dortmund, Jude Bellingham itatakiwa kuweka mezani kitita cha Pauni 100 milioni dirisha la usajili majira ya kiangazi, imeelezwa.

Bellingham amekuwa akiwindwa na miamba ya soka ya England ya Manchester United na Liverpool pamoja na Real Madrid ambao wana matumaini makubwa ya kumpata bila hofu yoyote.

Wikiendi iliyopita Dortmund iliendelea kusisitiza itafanya biashara na timu yoyote itakayoweka mezani kiwango cha pesa wanachokihitaji.

Mshahara wa sasa wa nyota huyo wa kimataifa wa England ni Pauni 300,000 kwa wiki na Dortmund wanaamini watapata timu itakayokuwa tayari kumsajili.

Hata hivyo, taarifa kutoka Ujerumani zinadai Madrid na Manchester City ndio zinazoongoza kuiwania saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 19.

Aidha Kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti hajazungumza lolote kuhusu tetesi hizo licha ya klabu yake kuhusishwa na kiungo huyo.

Muitaliano huyo ana viungo hatari kwenye kikosi chake kama Luka Modric, Aurelien Tchouameni, Eduardo Camavinga na Fede Valverde na alipoulizwa alisema: "Bellingham ni mchezaji mzuri na ameonyesha kiwango bora kwenye fainali za Kombe la Dunia

Qatar, lakini kuna wachezaji wengine hatari zaidi ya Bellingam." Kwa upande wa Man City itaongezea Pauni 75 milioni endapo watamuuza Bernardo Silva mwishoni mwa msimu, huku mkataba wa Ilkay Gundogun upo mbioni kuisha.

Dortmund iliweka mkazo kwenye usajili wa Bellingham kutokana na kiwango chake bora na haitakubali kumwachia kirahisi kama ilivyokuwa usajili wa winga anayekipiga Man United, Jadon Sancho.

Chanzo: Mwanaspoti