Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumekucha, Kispika cha Ahmed Ally charudi mtaani

KISPIKA BUGURUNI 1140x640 Kumekucha, Kispika cha Ahmed Ally charudi mtaani

Fri, 14 Oct 2022 Chanzo: dar24.com

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally leo Ijumaa ameanza kuwahamasisha Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo ili kufika kwa wingi Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam Jumapili (Oktoba 16), kwa ajili ya kuishangilia timu yao.

Simba SC itakabiliwa na mchezo wa Mkondo wa Pili Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Primeiro De Agosto ya Angola, huku ikiwa na mtaji wa mabao 3-1.

Ahmed Ally ameanza zoezi hilo katika Soko la Buguruni jijini Dar es salaam akiwa na baadhi ya vikundi vya Ushangiliaji na Mashabiki wa Simba SC walijitokeza kwa wingi.

Wapinzani wa Simba SC katika msicho huo, wanatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuanzi sasa, huku wakikabiliwa na mtihani wa kupindua meza wa kuwafunga wenyeji wao 2-0, kujihakishia kutinga Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba SC itatakiwa kulinda ushindi wake wa 3-1, kwa kusaka sare ama ushindi wa aina yoyote, ili itinge Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2022/23.

Hata hivyo Primeiro De Agosto imekua na Rekodi nzuri inapocheza ugenini, kwani mchezo uliopita dhidi ya Red Arrows ya Zambia iliambulia ushindi wa 2-1, kabla ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani kwao Luanda-Angola.

Chanzo: dar24.com