Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumekucha Firts League, vigogo wanne kibaruani

First League Kumekucha Firts League, vigogo wanne kibaruani

Sat, 21 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Msimu wa 2023/24 wa First League unatarajia kuanza leoJumamosi kwa mechi tano kupigwa viwanja tofauti, huku ikishuhudiwa timu nne zilizowahi kuwika Ligi Kuu zikifungua pazia hiyo.

Ligi hiyo ambayo zamani ilijulikana kuwa Daraja la Pili kabla ya kuitwa First League inashirikisha timu 16 ambazo zimegawanywa makundi mawili tofauti ikiwa kila upande utawatoa wababe wanne kucheza robo fainali kisha nusu hadi fainali.

Timu ambazo ziliwahi kukinukisha Ligi Kuu kabla ya kushuka daraja kwa misimu tofauti ni Alliance FC (Mwanza), Mwadui FC (Shinyanga), Rhino Rangers (Tabora) na African Sports 'Wanakimanumanu' ya jijini Tanga na African Lyon ya Dar es Salaam.

Katika ratiba ya mechi zitakazoanza leo, Kurugenzi ya mkoani Simiyu itakuwa wenyeji dhidhi ya Mapinduzi ya jijini Mwanza ambayo ndio msimu wao wa kwanza katika michuano hiyo, huku Mwadui ikiwa wenyeji wa Rhino Rangers huko Nyankumbu mkoani Geita.

TRA ya mkoani Kilimanjaro ambayo nao ni mara ya kwanza kucheza ligi hiyo, watakuwa nyumbani uwanja wa Ushirika Moshi, kuwakabili Alliance ya jijini Mwanza ambayo iliwahi kucheza Ligi Kuu na kushuka daraja msimu wa 2020/21.

Kundi B, itafungwa na Kasulu United ya mkoani Kigoma itakayowaalika Tanesco FC mchezo utakaopigwa uwanja wa Lake Tanganyika huku kila upande ukipigia hesabu ya pointi tatu.

Kundi A, itakuwa ni mechi moja tu, ambapo Nyumbu FC itawakabili African Lyon huku ratiba ikitarajia kuendelea kesho Jumapili kwa mechi tatu za Kiluvya dhidhi ya Dar City, Malimao kuwavaa Tunduru Korosho ilhali African Sports ikinyoshana na Lipuli 'African Wanderer’s'.

Meneja wa Malimao FC, Idd Mwambusi amesema ikiwa ni msimu wao wa kwanza katika ligi higo, wamejipanga kufanya vizuri na matarajio yao ni kupanda Championship, huku akiweka tahadhari kikosini.

Chanzo: Mwanaspoti