Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe msosi wa Alassane ni kawaida tu

Diao 91 1024x896.png Kumbe msosi wa Alassane ni kawaida tu

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji kinda mwenye umri wa miaka 20 na asili ya Senegal aliyesajiliwa Julai 2023 katika timu ya Azam FC, amecheza mechi mbili za ligi kati ya tano mpaka sasa akiwa hana rekodi ya kufunga bao hata moja.

Amekuwa gumzo kutokana na muonekano wake huku wengi wakiwa wamezoea kuwa wachezaji hawana miili mikubwa kama alionao pia yapo yanayosemwa kuhusu ulaji wake kutokuwa sawa na wenzake licha ya mashabiki kuonekana kutomuelewa mpaka sasa.

Mwanaspoti hili liliamua kufunga safari na kwenda kukutana nae ili kuweza kujua mengi kuhusu mshambuliaji huyo wa kigeni ambae anatumika eneo moja na wachezaji kama Prince Dube na Mbombo ambao wamekuwa na mafanikio msimu uliopita ndani ya timu hiyo.

Ushindani sio ishu

Alassane anasema ushindani sio kipao mbele chake kwani anachozingatia ni yeye kufanya kile kilichomleta ambacho ni kucheza hivyo kila anapopewa nafasi anataka kuitumia vizuri bila kuangalia nani huwa anatumika eneo hilo.

Timu kubwa kama Azam lazima iwe na wachezaji bora wengi na kocha anachagua yule ambae anadhani atamgfaa katika mechi husika huo kwake sio ushindani ila mpango wa kocha kwani hawawezi kucheza watu wote.

"Kila mmoja ni bora ukikosa namba kwa kipindi kirefu haimaanishi kuwa wewwe sio bora au umezidiwa ila ni mikakati ya mwalimu kutokana na mahitaji hivyo kwangu sioni ushindani wa namba ila timu iwez kuwa na wachezaji watakaoipa ushindi.

Ligi freshi tu

Hajaona utofauti wa ligi ya Senegali na huku kwani mambo mengi yanafanana ikiwemo ushindani wa timu kucheza kwa ubora ilikusalia katika nafasi nzuri ya msimamo kwani hakuna anaetaka kushuka au kufungwa mabao mengi.

"Hatujaachana sana ushindani ni ule ule bila kusahau wachezaji bora ambao wanapambania timu na namba za uhakika ili kuonyesha kile walichonacho ndani na nje ya nchi lakini bado nahitaji muda kwani nikiijua zaidi nitaweza kuonyesha utofauti."

Faida alizozipata

Tangia aanze kucheza ligi mwaka 2020 amepata mafanikio ambayo hawezi kuyasema wazi mbele za watu ndio maana anamshukuru Mungu kwa nafasi zote alizopata kutoka Senegali mpaka Tanzania kwaajili ya kucheza mpira hayo ni mafanikio makubwa.

"Sina cha kuwaambia maana ni mengi ila ipo siku nitayaweka wazi yote na ninaamini nitawashangaza wengi kwani bado mimi ni kijana mdogo mafanikio hayo yatawavutia na kuwafundisha wengi kuwa kila kitu kinawezekana."

Jezi namba 11

Anapenda kuchezea namba nyingine nje na hiyo ila kutokana na mahesabu ya kocha hana budi kukubaliana nayo na kuifanyia kazi na kuhakikisha anaitendea kazi ipasavyo na kuisaidia timu kufikia malengo bila kujali nafsi yake inapenda nini zaidi.

"Naifurahia zaidi jezi namba 12 kuliko zote nilizowahi kuchezea nahisi uhuru zaidi nikiwa na chezea nafasi hiyo ila lazima tuheshimu maamuzi ya kocha kwani yeye anajua zaidi yetu na niko kazini siwezi kuwa na machaguo ya nini nataka kufanya,"anasema mshambuliaji huyo.

Biashara iko moyoni

Anasema hajawahi kufikiria kuacha mpira au asingekuwa mchezaji angefanya nini kwani tangu utotoni alishajijua kuwa hapendi kusoma ndio maana akakomaa na soka kwani aliona ndio jambo pekee linalomfanya kuwa huru.

"Napenda hela hivyo biashara ungekuwa mpango wa pili kama soka linge ni kwamisha kwa sababu darasani sikuwa vizuri ndio maana naona bila mpira sijui ingekuaje na kama ningeshindwa basi ningehamia upande mwingine kikubwa mkono uende kinywani na mfuko uwe mzito ili maisha yaende vizuri."

Msosi balaa

Anasema ulaji wake ni wa kawaida nje na maneno yanayosemwa kuwa anakula kuku wa nne na chapati nyingi kuliko wachezaji wengine wakati sio kweli,"Nakula kama wengine tu kipande cha kuku."

Namba ya kiatu

Alanasse anasema namba ya kiatu anachovaa kimekuwa gumzo kwa watu wengi ukizingatia na umri alionao ila anachoshangaa kwa upande wake ni namna wanavyomuona mdogo lakini anavaa saizi hiyo jambo ambalo ni la kawaida.

"Mimi ni kijana mkubwa sasa ndio maana nimetoka nyumbani mbali huko na kuja kufanya kazi huku hivyo sio jambo la ajabu kuvaa kiatu namba 45."

Mtoto wa mama

Anasema yeye ni mtoto pekee wa kiume hivyo kuwasiliana nae ni kawaida ila sio mara zote kama ninavyowasiliana na rafiki yangu wa kike.

"Nikiamka asubuhi tu mtu wa kwanza ni mchumba wangu hivyo huyo ni zaidi ya mama kwahiyo siwezi kusema mimi ni mtoto wa mama ila nawasiliana nae kwani najua niko mbali na anataka kujua hali yangu."

Wanangu sana

Anasema wachezaji wengi wamekuwa marafiki zake japokuwa lugha ndio imekuwa changamoto kubwa ila upendo wa dhati uliopo katika timu hii kunamfanya awe huru zaidi pindi anapokuwa nao kambini na mahali pengine.

"Wako wengi ila Sopu,Sidibe,Pascal,Sebo na Akaminko wamekuwa karibu zaidi ya wengine ambao kwa namna moja au nyingine wamechangia furaha na amani ya kufanya kazi nao kuongezeka."

Muda wa ziada

Kinda huyo anasema muda wake wa ziada anapenda kufanya mambo yanayompa furaha na kumpotezea mawazo.

"Napenda kuchati na watu ninaowapenda na kwenda sehemu za starehe kama maeneo yenye mziki mkubwa na chakula kizuri kama kuku na vya asili yetu bila kusahau kutembea mazingira kama Kariakoo na mengineyo hapa Dar es salaam."

Chanzo: Mwanaspoti