Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe 'bleach' za Pacome ndo' zilisababisha Maseke amtwange Rasta

Kipigooo 0011 Kumbe 'bleach' za Pacome ndo' zilisababisha Maseke amtwange Rasta

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ubora wa Kiungo wa Yanga Pacome Zouzoua raia wa Ivory Coast kuzalisha mashambulizi mara kwa mara kwenye lango la mpinzani umesabaisha wachezaji wawili wa timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni ’KMC’ kutwangana Makonde ‘Live’ uwanjani.

Tukio la kustaajabisha lililoshuhudiwa ‘Mubashara’ na watazamaji wa mechi hiyo ya Ligi Kuu ya NBC katika Dimba la Jamhuri na wale waliokuwa wakitazama kupitia runinga, lilitokea Jumamosi iliyopita, Februari 17, 2023 dakika ya 36 ya mchezo huo ambapo kipa wa KMC, Wilbol Massawe alilushiana Makonde na winga wa kulia wa timu yake, Ibrahim Elias ’Rasta’.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari kutoka Morogor ambaye alishuhudia ugomvi huo mwanzo mwisho, amesema chanzo cha ugomvi huo ni Kiungo wa Yanga Pacome kuzalisha mashambuliaji mara kwa mara kwenye lango la Watoza Ushuru hao wa Kinondoni, waliotumia kanuni ya TFF Kuhamisha mchezo huo kutoka Dar kwenda Morogoro.

Mara kwa mara kipa huyo alimuelekeza Rasta huyo aliyeamua kutoka mbele kwenye nafasi yake kuja nyuma kusaidi ulinzi wa kumchunga Pacome.

Winga huyo alipoona lawama zinazidi hasira zimepanda naye kaamua kumfokea kipa huyo akidai kazi yake si ya ulinzi, kwamba ameamua kujitoa kushuka chini kuimalisha ulinzi wa kubani safu hiyo kali ya washambuliaji wa Yanga.

Hivyo kitendo hicho cha kufokewa mara kwa mara kimemkera na kuamua naye kumfokea kipa huyo. Kipa huyo kwa hasira ya kufokewa alijibu mashambulizi kwa kumsukuma Elias aliyekosa stamina kuanguka chini.

Rasta huyo alipoinua alijibu mashambulizi kwa kumtwanga konde la uso Kipa wake huyo kabla na Nahodha wa timu hiyo Awesu Awesu kutumia mamlaka yake ya Uongozi ndani ya Uwanja na kumtuliza kipa huyo huku beki Andrew Vicent’Dante’ naye akibeba jukumu la kumtulia Elias.

Katika hali ya kushangaza refa Mdowe kutoka Tanga hakuwapa adhabu yoyote wachezaji hao kwa kosa la kuchapana makonde uwanjani badala yake alisikika akisema ”Oya tatizo nini chezeni mpira” baada ya kusema hivyo refa huyo aliamuru gemu kuendelea.

Kitendo cha wachezaji hao kutwangana makonde kilionekana kuwachefua makocha wa timu hiyo ambapo mara baada ya ugomvi huo kuamuliwa walimuinua kipa wa hakiba Denis Richard aliyeingia kuchukua nafasi ya Kipa Massawe.

Mchezo huo wa raundi ya 16 ulimalizika kwa KMC kuambulia kichapo cha bao 3-0, mabao mawili ya Yanga yakifungwa na kiungo Mudathir Yahya Abbas na bao la mwisho likifungwa na Pacome Zouzoua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live