Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe 'Pacha wa Fei Toto' aliyetua Yanga walimtaka Simba!

Shekhani Yanga Shekhan Ibrahim.

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga SC imelipa kisasi nje ya uwanja mbele ya watani wao Simba baada ya kufanikisha kumsajili kiungo mmoja kinda fundi kutoka Zanzibar na kuwaacha jamaa zao wamechanganyikiwa.

Iko hivi. Simba ndio walikuwa wa kwanza kumfuata kinda mmoja Shekhan Ibrahim Khamis ambaye kule Zanzibar anatambulika kama kijana mwenye kipaji kikubwa kuwahi kutokewa kisiwani humo.

Shekhan ambaye alikuwa mchezaji wa JKU ya Zanzibar ambayo alitokea Feisal Salum 'Fei Toto' akitambulika kama mchezaji mwenye kipaji kikubwa akimudu kucheza kama kiungo mchezeshaji na mshambuliaji na winga zote mbili.

Simba ilikuwa tayari imeshamtumia mpaka ya boti ili atue mapema jijini Dar es salaam kumaliza dili hilo, lakini Yanga wakafanya umafia mmoja wa fasta.

Yanga wao baada ya kusikia taarifa hizo za Simba wakabadili gia wakimtumia tiketi ya ndege iliyomuwahisha mjini na kusaini mkataba huo wa miaka mitatu.

AMEPIKWA KWENYE AKADEMI

Kipaji cha Shekhan kilianzia kwenye akademi ya JKU kisha msimu huu akapandishwa kuja timu kubwa na kuanza kuchanganya akiwa pia kwenye timu za taiga hilo za taifa chini ya miaka 18.

Kwa mujibu wa kocha wa JKU Msellem Sultan Hemed ameliambia Mwanaspoti kando ya Fe toto tishio lingine litakuja kuwa Shekhan ambaye ana kipaji kikubwa na kwamba Yanga imepata mchezaji mdogo bora kwa baadaye.

"Huyu naweza kusema atavuma kuliko Fei toto, hawa wote nawajua ni wachezajoi bora lakini kitu ambacho Shekhan anazidi ni namna ambavyo ana mudu kucheza nafasi nyingi na kwa uwezo mkubwa, Yanga wamepata mchezaji hasa," alisema Hemed.

Mwanaspoti linafahamu Yanga wanasubiri tu kufunguliwa kwa dirishas dogo la usajili ili wamtambulishe kinda huyo.

Mbali na Simba klabu nyingine iliyokuwa inavizia saini ya Shekhan ni Azam na Coastal Union ya Tanga ambao tayari walikuwa wanafanya mazungumzo ya siri na wasimamizi wa kiungo huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live