Unaweza ukaona ni kawaida kwa Fabrice Luamba Ngoma kucheza pamoja na Clatous Chama katika kikosi cha Simba halafu ukaona ni kawaida tu wawili hao kukutana na wala hakuna kitu ambacho kimewahi kutokea.
Sasa ipo hivi unaambiwa kuwa kiungo wa Simba Fabrice Ngoma ameweka wazi kuwa mmoja kati ya wachezaji ambao anawakubali kabla ya kutua Simba basi ni Clatous Chama.
Lakini pia kiungo huyo pia ameweka wazi kuwa mchezji huyo anamkumbuka kutokana na aliwahi kumpa machungu ambayo hajawahi kuyasahau katika historia ya mpira wake.
Ngoma anasema kuwa Chama anamkumbuka zaidi kutokana na kuwahi kuwafunga bao ambalo liliwafanya washindwe kufuzu kwenda hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika msimu wa mwaka 2018/19.
Katika msimu huo Simba ilifuzu kwenda robo fainali baada ya kuwafunga AS Vita katika mchezo wa mwisho wa makundi ya ligi ya Mabingwa kwa idadi ya mabao 2-1 ambapo bao la mwisho na laushindi kwa Simba lilifungwa na Clatous Chama dakika za mwisho kabisa za mchezo.
Bao la kwanza la AS Vita lilifungwa na FRANCIS KAZADI KASENGU, mchezo wa kwanza ambao AS Vita walikuwa nyumbani walishinda kwa mabao 5-0.