Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe KMC waliipania Yanga!

Yanga 3 Pic Data Kumbe KMC waliipania Yanga!

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

EBWANA eeh! kumbe kwenye mchezo wa juzi Jumamosi uliowakutanisha Yanga na KMC Kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, watoza ushuru hao wa Kinondoni walikuwa wamepania.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Kocha Msaidizi wa KMC, Habibu Kondo aliweka wazi kuwa walikuwa wamepania kupata matokeo chanya katika mchezo huo kulingana na kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa Octoba 25 mwaka jana kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

"Tulipaswa kushinda mechi hii. Tulitengeneza nafasi nyingi lakini katika eneo la umaliziaji umakini ulikua mdogo, nadhani wachezaji wetu walikuwa na presha kubwa kwenye mchezo huu kwasababu toka tupo kambini tuliwaeleza kuwa huu ni mchezo wa kisasi kwani Yanga walitufunga mechi ya kwanza hivyo tulitaka tushinde hii ili tuwe sawa.

Yote kwa yote tunashukuru kwa matokeo haya tuliyoyapata na sasa tunarudi kwenye viwanja vyetu vya mazoezi kujipanga kwa michezo ijayo," alisema Kondo.

Hata hivyo KMC hawana rekodi nzuri ya kuifunga Yanga kwani tangu imepanda daraja msimu wa 2018/19 imeweza kushinda mechi moja tu kwenye Ligi kati ya sita timu hizo mbili zilizokutana huku Yanga wakishinda mara tatu na kutoa sare mara mbili.

KMC ipo nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi na alama 36 baada ya kucheza mechi 25 kushinda 10 sare sita na kupoteza sita na mchezo ujao watakuwa nyumbani Aprili 16 kupepetana na Gwambina iliyo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi.

Related Simba SC, Yanga zapewa mchongo Mastaa Yanga wachimba mkwara! Lyanga atuma salamu, akitaka kiatu cha dhahabu

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz