Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe Diarra alimuumiza Kibu kwa maksudi?

Kibu X Diarra Faini Kumbe Diarra alimuumiza Kibu kwa maksudi?

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa habari na Mawasilino Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa watani zao Yanga walimuumiza kwa maksudi Kibu Denis baada ya kuona ndiyo mchezaji pekee aliyekuwa akiwasumbua katika mchezo wa Dabi ambao leo unatimiza mwezi mmoja.

Kibu D aliumia kipindi cha pili cha mchezo huo baada ya kugongana na kipa wa Yanga, Djigui Diarra wakati wa harakati za kuwania mpira kwenye lango la Yanga.

"Kibu Denis aliumizwa makusudi kabisa kwa sababu alikuwa mwiba kwao. Hakuna neno jingine lolote la kusema zaidi ya kusema ni makusudi kabisa Kibu ameumizwa, walidhamiria, walitumwa kwenda kumuumiza Kibu D.

"Kibu ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa sana, angesalia pengine tungekuwa tunazungumza lugha nyingine. Kibu aliumia enka akatolewa nje, mchezo wa namungo ataukosa kwa sababu madaktari wameshauri apumzike ilia pone kabisa.

"Sadio Kanoute naye ameumizwa kwenye mchezo huo kwa makusudi katika. Madaktari wameshauri apumzike angalau mchezo mmoja ili apone na kurejea katika utimamu kamili," amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live