Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe Bacca amerithi soka kutoka kwa mshua!

Bacca Baba Kumbe Bacca amerithi soka kutoka kwa mshua!

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mzee Abdallah Hamad, ambaye ni baba mzazi wa beki wa Kati wa Yanga, Ibrahim Hamad Abdullah Bacca amesema kuwa mwanaye huyo amerithi kipaji cha kucheza soka kutoka kwake.

Bacca ambaye ni mchezaji wa Yanga kwa sasa, pia ni mwajiriwa wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM).

“Mimi nilikuwa mchezaji hatari sana, nimecheza timu ya Chuo cha Mafunzo kwa miaka 11, timu hiyo ilikuwa Ligi Kuu ya Zanzibar. Mimi nimezaliwa Pemba lakini nilikuja Unguja kwa ajili ya mpira tu, kwa hiyo Ibrah amerithi kwangu, hajabahatisha.

“Mimi nilikuwa winga wa kulia na kushoto na ninatumia miguu yote miwili kama anavyotumia yeye. Nilitamani acheze straika lakini akasema mimi nataka kuwa beki. Ninaye mwingine mdogo ila yeye ni starika, bado vitu vipo ila nakuza mwenyewe.

“Nilimwambia Ibrah kukaa benchi sio tatizo, kila jambo linahitaji subira na sibira ndiyo kila kitu, hakuwa na pupa, nadhani leo mnaiona shughuli yake ni ya kikamanda, sio ya kitoto. Kila mmoja anamzungumzia Ibrahim Bacca,” amesema Mzee Hamad.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: