Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe Aucho naye aliumia siku moja kabla ya kuwavaa Belouizdad!

Khalid Auchoooooooo Kumbe Aucho naye aliumia siku moja kabla ya kuwavaa Belouizdad!

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imefahamika kuwa, kiungo mkabaji wa Klabu ya Yanga raia wa Uganda, Khalid Aucho aliumia mazoezini siku ya Ijumaa ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo wao wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.

Hayo yamesemwa leo na Ofisa Habari wa Kikosi cha Yanga, Ally Kamwe wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kuelekea mchezo wao wa mwisho wa makundi dhidi ya Al Ahly.

Licha ya kuumia, Aucho aliona si vyema kukaa nje, badala yake akamuomba Kocha Gamondi ampange ili kumsapoti mchezaji mwenzake, Pacome ambaye pia alikuwa ameumia lakini alicheza.

Mastaa hao walicheza mchezo huo dakika zote 90, na kuonesha viwango bora na kuisaidia timu yao kushinda bao 4-0 na kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

“Daktari wa mpira, Khalid Aucho, Ijumaa kabla ye kwenda kwenye mechi Jumamosi, aliumia. Lakini mwanaume akasema hapana, mashabiki wa Yanga wanataka kwenda robo fainali, mashabiki wanataka kuiona Pacome Day, akasema na mimi nimo.

“Hii wiki Yanga tumepitia mazito sana lakini Mwenyezi Mungu alikuwa upande wetu kila kitu kikaenda vizuri. Kama mhamasishaji unapoona jambo lako linawaingia mpaka wachezaji wote kambini, ujue sio jambo dogo, ni jambo kubwa na umefanikiwa pakubwa. Pacome Day ilifana sana,” amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live