Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuku: Mechi za CAF zimenijenga

Ahmad Waziri Kuku Kuku: Mechi za CAF zimenijenga

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beki mahiri wa Singida Big Stars, Hamad Waziri ‘Kuku’ amesema kitendo cha kucheza mechi za Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na kikosi hicho imemsaidia kumuongezea maufundi dhidi ya mastaa katika Ligi Kuu, japo timu hiyo ilikwamba kutinga makundi kwa kung’olewa na Future ya Misri.

Waziri amepata nafasi za kucheza mechi mbili za raundi ya pili ya michuano hiyo dhidi ya Future na kutolewa kwa jumla ya mabao 5-2, ikishinda nyumbani 1-0 na kulala ugenini 4-1.

“Kule ujue unacheza na washambuliaji ambao wana uzoefu, halafu wana ujanja mwingi sana kuliko mimi, nimejifunza namna ya kukabiliana na washambuliaji hatari katika mazingira yoyote yale,” alisema Waziri na kuongeza;

“Ukicheza mechi kubwa dhidi ya Wamisri kwa namna moja ama nyingine akili yako lazima ikue, hivi ndivyo najivunia, hata kama tumetolewa mapema na kushindwa kutinga makundi.”

Akizungumzia maendeleo ya afya yake baada ya kuumia dhidi ya Simba, alisema atakuwa nje kwa wiki tatu.

“Nilichana nyama za paja kwahiyo nimepewa mapumziko ya wiki tatu ili nikae sawa. Kweli kuna ushindani wa kutosha kikosini tangu nikiwa sichezi, kwa sasa nimeanza kucheza nimeumia ila nachukulia kawaida kwa sababu tulicheza mechi nyingi bila kupumzika,” alisema.

Waziri alianza kucheza mechi za Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Future FC zote mbili.

Chanzo: Mwanaspoti