Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Kujiamini, Ubora vimetuangusha" - Kocha Simba Queens

Simba Simba Simba Wachezaji wa simba Queens wakiwa uwanjani dhidi ya Vihiga Queens

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kupokea kipigo cha bao 2-1 na kuenguliwa katika mashindano ya CECAFA, kikosi cha Simba Queens kimeyakubali matokeo kama sehemu ya kujifunza na wanatazama mbele kwa michuanao ijayo.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo ,kocha mkuu wa Simba Queens Hababuu Omar amesema Kujiamini na ubora wa wapinzani wao ndio sababu kubwa iliyowafanya kutolewa katika mashindano hayo.

"unajua sisi tulienda kwa hofu katika mchezo ule lakini wenzetu walikuja wamejiamini kabisa pasipo kuwa na hofu dhidi yetu wala hawakuona athari yetu"

"lakini kubwa nimejifunza ili ufanikiwe unahitaji kuwa na kikosi imara cha wachezaji wa daraja la juu sio wale wa kawaida kawaida, mfano sisi ukitoa wachezaji kumi na moja wanaobaki hawalingani viwango na wenzetu" amesema hababuu

Kikosi cha Simba Queens kinajiandaa kwa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu baada ya kuenguliwa na Vihiga Queens katika hatua ya nusu fainali, katika mchezo huo watakutana na Lady Doves WFC ya Uganda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live