Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuisifia Simba ni unafiki uliopitiliza - Mchambuzi

Simba Warejea Nchini, Kituo Kinachofuata Ni Kagera Sugar Kuisifia Simba ni unafiki uliopitiliza - Mchambuzi

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka kutoka Clouds FM, David Kampista amesema kuwa kuisifia Klabu ya Soka ya Simba ni unafiki kwani licha ya ujio wa kocha mpya lakini hakuna mabadiliko yoyote chanya ya kiuchezaji.

Kampista amesema hayo mara baada ya vijana hao ambao kwa sasa wananolewa na Kocha Benchikha kufungwa bao 1-0 katika mchezo wao wa ugenini wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca nchuini Morocco.

"Tunaipaka mafuta tena kwa mgongo wa chupa, binafsi siwezi kuisifia Simba kwa mechi ya jana utakuwa ni unafiki uliopitiliza. Kwa mtazamo wangu Simba wamejaribu kujitutumua kutokana na hali waliyonayo.

"Bado ujio wa Kocha mpya umewashtua tu wachezaji ambao wanaiwazia hatma yao baada ya msimu kumalizika kwa kuwa lazima mikataba ya baadhi yao inakaribia kumalizika

"Wanapambana tu lakini ukweli ni kwamba kiwango chao kwa sasa hakiwezi kuivusha Simba katika daraja refu la kucheza nusu fainali ya Klabu bingwa Afrika.

"Naona watu wanaimwagia sifa Simba kwa mechi ya jana, ghafla wamesahau Simba walijitutumua dhidi ya Wydad ambaye ana shida zake laki tisa milioni na bado Mnyama akafa katika mechi yenye hesabu kali kupita mfano.

"Kwa kifupi tangu msimu uliopita Simba alifuzu robo fainali kwa tabu mno! Lakini bado wenye timu ni kama hawakujifunza kwa aina ya sajili wanazozifanya, mwisho wa siku mzigo wa lawama huwa unabakia kwa makocha.

"Simba kwa sasa sajilini katika Klabu zinazocheza makundi katika michuano hii mara kwa mara na sio kuokoteza au kununua maveterani mnajiumiza wenyewe. Mpeni Benchikha madirisha kadhaa awatengenezee timu, mkichelewa anguko lenu halipo mbali," amesema David Kampista.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live