Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuiona Al Merrikh vs Yanga Tsh 100,000

Yanga Rekodi Mpyaaaaa.jpeg Kuiona Al Merrikh vs Yanga Tsh 100,000

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kesho kitapaa nchini kuwafuata wapinzani wao nchini Rwanda, El Merreikh ya Sudan kwenye mchezo wa hatua ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika utapigwa Septemba 16 saa 10:00 jioni.

Viingilio katika mechi hiyo iytakayopigwa kwenye Uwanja wa Pele ambako El Merreikh wamechagua kuwa Uwanja wao wa nyumbani, vimetangazwa huku kiingilio cha juu kikiwa Sh104,391 ya Tanzania (Franc 50,000), kinachofuatia ni Sh52,195 (Franc 25,000) na cha chini ni Sh20,870 (Franc 10,000).

Yanga ilifuzu hatua hiyo kwa ushindi wa jumla ya mabao 7-1, baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kushinda 2-0. El Merreikh ilifuzu kwenda hatua ya kwanza ya mtoano kwa faida ya bao la ugenini baada ya kulazimishwa suluhu hiyo ya bila kufungana ambapo awali walitoka sare ya bao1-1 dhidi ya Otoho d'oyo ya Congo Brazzaville.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: