Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuifanya fitina Yanga ni ngumu, hata wasiposajili wanachukua tena

Hersi Yanga Gamondiz Yanga wakishangilia ubingwa

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka kutoka TV3, Boiboi Mkali amesema kuwa kuwafanyia fitina Klabu ya Yanga kwa sasa ni vigumu kutokana na uimara wa uongozi walio nao.

Boiboi amedai kuwa kutokana na mikakati waliyo nayo mabingwa hao wa muda wote wa Ligi Kuu ya Tanzania, wanao uwezo wa kuchukua ubingwa huo kwa miaka miwili mingine hata kama hawatafamnya usajili wowote.

"Hii Yanga inaweza isifanye usajili kwa miaka miwili na bado ikaendelea kuchukua ubingwa kwa misimu mingine miwili mfululizo kikubwa wahakikishe tu wachezaji ambao wapo sasa hivi wanabaki kikosini.

"Hiki ni kikosi ambacho kimetimia kila sehemu kuanzia nyuma mpaka mbele wapo vizuri hivyo wanaweza kuendelea ku dominate ligi yetu kwa misimu mingine miwili mfululizo kwa kubeba makombe.

"Hakuna mchezaji anayeweza kuondoka kwenye klabu ambayo ina Kila kitu ambacho mchezaji anahitaji, inabeba Mataji, inalipa vizuri lakini kubwa zaidi ina malengo mazuri kama timu.

"Yanga wanapoenda kumsajili mchezaji wanamueleza mipango ya klabu na kumuelekeza nini malengo Yao kwake, wakati Simba inaifanyia fitina Yanga walikuwa wapo vizuri Kwa hiyo ilikuwa rahisi kuwafanyia fitina lakini sio Kwa Yanga hii ya saaa ambayo imetimia kila idara," amesema Boiboi Mkali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live