Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuhusu viporo! Tuheshimu uamuzi wa Bodi

Almasi Kasongooo Almasi Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi.

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viporo vya mechi za ligi huwa na pande mbili inategemeana na aina ya matokeo ambayo yatapatikana katika mechi hizo. Na hata uungwaji au kutoungwa mkono kwa mechi za viporo kunategemea na namna upande husika utakavyonufaika au kuathirika baada ya mechi kuchezwa.

Kwa mfano, ikiwa timu yenye viporo itapata ushindi, ni vigumu kusikia watu wa upande wake wakikosoa uwepo wa viporo kwenye ligi yetu tena watatoa kila aina ya utetezi kuhalalisha uwepo uamuzi wa kusogezwa mbele kwa mechi zao.

Lakini kwa upande ule ambao timu yake itafanya vibaya au hautoona kunufaika na mechi za viporo za timu fulani, hauwezi kufurahia na hapo utasikia lawama kuwa uwepo wa mechi hizo za viporo ulilenga kuinufaisha timu fulani ili itwae ubingwa au ipate manufaa fulani.

Hili sio geni na limekuwa likitokea mara kwa mara kwenye ligi yetu na mara nyingi wanaobebeshwa lawama huwa ni Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi (TPLB).

Ligi yetu msimu wa 2023/2024 umeshaanza na tayatri suala la viporo limeshaanza kuwa mjadala baada ya taarifa kuwa Simba imeomba mechi yake dhidi ya Coastal Union ichezwe leo ili baadaye isije kuwa na viporo vingi pindi itakapokuwa na kibarua cha kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na African League.

Kama kawaida yetu, kuibuka tu kwa taarifa hizo kumesababisha kuwepo kwa makundi mawili ambayo moja linasapoti uamuzi wa kuomba mechi hiyo ichezwe Ijumaa na lingine halisapoti mechi hiyo ichezwe leo.

Na kwa hali halisi, mechi hiyo haitachezwa na habari za ndaani zinathibitisha kuwa maombi ya Simba yametupiliwa mbali. Sasa wito wangu tu ni kwamba kama leo uamuzi wa Bodi ya Ligi unaheshimiwa, yakitokea kesho pia uheshimiwe hivyohivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: