Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuhusu kuinoa Man U... Mourinho amtabiria Southgate

Gareth Southgatee Kocha wa England, Gareth Southgate na Phil Foden

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Jose Mourinho ametabiri Gareth Southgate ana uwezo wa kufanya kazi yoyote baada ya kipindi hiki anachohusishwa na mpango wa kwenda kuinoa Manchester United.

Man United kwa sasa ipo chini ya kocha Erik ten Hag, hata hivyo, Mdachi huyo anaonekana kuirudisha timu hiyo nyuma na kuwaondoa kwenye orodha ya klabu kubwa Ligi Kuu England. Kwa sasa timu hiyo ipo nyuma ya Top Four kwa pointi 11, hivyo kushindwa kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, itakuwa habari mbaya kwa kocha huyo wa zamani wa Ajax.

Wakati mmiliki mpya bilionea Sir Jim Ratcliffe akiwa bado hajafanya uamuzi wa kuhusu hatima ya kocha huyo, kumekuwa na makocha wengi wanahusishwa na kibarua cha timu hiyo ya Old Trafford.

Southgate ni kocha mwingine anayehusishwa na miamba hiyo. Kocha huyo wa timu ya taifa ya England, huenda akaachana na timu hiyo baada ya fainali za Euro 2024 kufika tamati, licha ya mkataba wake kufika tamati Desemba.

Na Mourinho anadai kwamba Southgate anaweza kufanya kazi yoyote ile baada ya kupata uzoefu mkubwa kwenye kuinoa timu ya taifa ya nchi yake.

Na Southgate alisema: "Nilikuwa na miaka 35 wakati nilipoinoa timu ya Ligi Kuu England na nilimaliza nafasi ya 12 na 13. Sikuwa nafahamu vitu kama ninavyovifahamu kwa sasa. Nakumbuka nilizungumza na Mourinho na yeye aliniambia, utakapomaliza kazi yako unayofanya kwa sasa, basi utakuwa na uwezo wa kufanya kazi yoyote hapa duniani. Nadhani alikuwa sahihi."

Chanzo: Mwanaspoti