Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kugombania namba kunaniimarisha - Dickson Job

Miguel Gamondi Xx Dickson Job Kugombania namba kunaniimarisha - Dickson Job

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki kitasa wa Klabu ya Yanga, Dickson Job amesema kuwa hali ya kuwa kwenye kikosi chenye mabeki wengi wakubwa wanaogombania namba, inamsaidia kumuimarisha ili aweze kufanya makubwa zaidi.

Job amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya KMC ambapo alifanikiwa kufunga bao la ufunguzi wa Ligi kwa timu yake.

"Mchezaji kupata changamoto ya namba ni kitu kizuri kwa sababu inakufanya ujitume zaidi na kuongeza ubora ili uonyeshe ulicho nacho.

"Competition kama hii ni nzuri kwa sababu kila mtu anapopata nafasi lazima ajitolee ili kufanya vizuri na kumshawishi mwalimu. Hii inatuongezea nguvu kwenye timu na kutufanya tufanye vizuri katika timu yetu," amesema Job.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: