Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kufuzu kwa Yanga Robo Fainali ashukuriwe Mo Dewji - Ahmed Ally

Kufuzu Kwa Yanga Robo Fainali Ashukuriwe Mo Dewji   Ahmed Ally Kufuzu kwa Yanga Robo Fainali ashukuriwe Mo Dewji - Ahmed Ally

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Semaji la CAF, Ahmed Ally amesema, mafanikio wanayoyapata Yanga SC yanategemea sana jinsi Simba walivyotangulia kujidhatiti.

Amema kama si Mo kuamua kuwekeza basi pengine Yanga isingefika ilipo.

“Kufuzu kwa Yanga SC katika hatua ya robo fainali wa kushukuriwa ni Rais wa heshima wa Simba ni Mohammed Dewji na wa pili ni Simba SC.

"Wakati Mo anakuja kuwekeza Simba alisema vision yake ni kushinda ubingwa wa Afrika na baada ya hapo tukaanza mchakato wa kutawala soka la Afrika.

"Wakati Mohammed Dewji anatengeneza dira ya kutawala soka la Afrika vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa pono, vilikuwa haviwazi kushindana Afrika na kusumbua.

Baada ya miaka mitano ndio na wengine wameamka na wenyewe kutaka kuanza kufanya vizuri. Kama Simba SC na Mohammed Dewji tungeendelea kulala basi hadi sasa hakuna klabu yoyote Tanzania ingekuwa na hasira, malengo ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika ndio maana nasema robo fainali yao ya kwanza wa kushukuriwa ni Mohammed Dewji ndio aliwaamsha watu kutoka kwenye usingizi. Huu ndio ukweli ambao utadumu milele.” alisema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live