Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kufungwa na Morocco ni Ibada tosha

Tanzania Morocco.png Kufungwa na Morocco ni Ibada tosha

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa Kiwango chetu Tumejitahidi.

Kipindi cha Kwanza

Stars bila mpira walikuwa wanazuia kwenye muundo wa 5-4-1,malengo makuu katika muundo huu yalikuwa ni

1.Kuzuia hatari ya Morocco Pembeni ya uwanja na

2.Katika ya uwanja wakati Morocco wana mpira (On Ball).

Stars kwenye muundo wa kuzuia wa 5-4-1,Kibu Denis alibaki pekee kwa ajili ya kuweka presha kwenye muundo mdogo wa Morroco wa kutengeneza mashambuli ambao ni 1+3+2.

Kwenye muundo wa kujenga mashambuli wa Morocco wa 1+3+2,Mabeki wawili wa Morocco Saiss na Agued walikuwa huru sana kwenye kuanzisha mipira mingi kwasababu Kibu muda mwingi ilibidi aanze kupress mbele ya uso wa Amrabat.

Stars kwenye mistari miwili ambayo ilikuwa kwenye muundo wa 5+4 walifanikiwa sana kuzuia hatari nyingi kwasababu wachezaji tisa walikuwa wanazuia nyuma ya mpira muda mwingi.

Ni kama Ziyech aligundua njia rahisi ilikuwa ni kutumia nafasi kubwa (space) iliyokuwa inaachwa katikati mwa uwanja mbele ya muundo wa kuzuia wa Stars ambao ni 5+4,wakati Stars wanasubiri kujibu maswali ya 1+3+2 ya Morocco kwenye kuanzisha mashambuli.

Stars walishindwa kabisa kujibu maswali ya Morroco wakati hawana mpira,kwasababu Morocco walikuwa wanazuia vizuri 4-2-3-1 na Stars ilikuwa haina wacheza wengi wabunifu katikati mwa wakuutoa mpira vizuri kwenye safu ya ulinzi na kuupeleka mbele.

Kipindi Cha Pili.

Mabadiliko ya kumtoa Himid Mao, na Mourice kisha Samatta na Msuva kuingia ilimaanisha Stars walikuwa wanataka kuongeza matendo ya kushambulia kwenye zone ya mwisho ya uwanja.

Kiasi mabadiliko haya yalikuwa na tija kwasababu kuna baadhi ya matukio ya kupata nafasi kwenye eneo la mwisho yalitokea.

Ukicheza na timu aina ya Morocco ukijisahau kidogo utaadhibiwa,dakika chache za kushindwa kumzuia Ziyech kupiga pasi kwenye Ile half space na ku cover half goli la kujifunga likatokea.

Note

Charles M'Mombwa ana kipaji kikubwa, anahitaji muda na kuaminiwa.

Amrabat alikuwa anafanya anavyojisikia mbele ya Saiss na Agued.

Haji Mnoga anatukumbusha ulaya Kuna kitu.

Adel Amrouche tactically alikuwa superb.

Full-time

Stars 0-2 Morroco

Kufungwa na Morocco ni Ibada tosha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live