Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuelekea Game ya Namungo na Mbeya Kwanza

FC Namungo.jpeg Namungo FC

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Namungo FC walishinda katika mechi yao mwisho ya ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting, ulikuwa ni mchezo uliobeba hatma ya benchi lao la ufundi, waliingia uwanjani wakiwa na mentality hiyo na wakapata ushindi.

Kama kuna sehemu ambayo inawaangusha sana Mbeya Kwanza ni eneo lao la ulinzi, linapitika kirahisi mno na wanaruhusu magoli mara kwa mara, ni ngumu kushinda mechi ya mpira wa miguu kama timu inakosa balansi katika maeneo muhimu.

Inaweza kuwa ni mechi baina ya ubora wa kushambulia wa Mbeya Kwanza dhidi ya uimara wa kuzuia kwa Namungo, bila shaka Namungo wanakwenda kukutuna na mtihani mgumu hasa ukitazama kuwa wanashida pia ya kuruhusu magoli.

Katika mechi tano za mwisho wamepata clean sheet moja, ni wastani mbaya ukitazama wanakwenda kucheza dhidi ya timu ambayo haifajanikiwa kufunga goli lolote katika mchezo mmoja tu kati ya mitano ya mwisho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live