Staa wa Ajax, Mohamed Kudus anatarajiwa kuwasili England wikiendi hii kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na West Ham kwa dau la Pauni 38 milioni na kusaini mkataba wa miaka mitano.
West Ham imefikia uamuzi wa kumnunua kiungo huyo fundi aliyeonyesha kiwango bora kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwa kutumia pesa ilizopata katika mauzo ya kiungo wake Declan Rice.
Awali Kudus alidaiwa kuwa kwenye rada za Brighton lakini klabu hiyo ilishindwa kumpata kutokana na kushindwa kufikia muafaka kwenye masuala ya ada ya uhamisho.
Staa huyu wa kimataifa wa Ghana, msimu huu amefunga mabao manne kwenye mechi tatu za michuano yote.