Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kucheza na Yanga ni mateso - Kocha Kagera

Tano Ta Yanga Yanga wakishangilia ushindi

Tue, 7 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, Marwa Chamberi amesema kuwa mchezo wa kesho wa ligi dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga utakuwa mgumu kutokana na kwamba waliwazuia kupata ushindi katika duru ya kwanza kule Kaitaba Stadium.

Chamberi amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.

“Tupo kwenye Ligi moja na Yanga lazima tucheze nao na kucheza na Yanga ni mtihani, unajipima standard yako kama amemfunga huyu ukicheza nae wewe unajua ubora wako kwenye ligi uko wapi. Walimu tunataka kuwa bora ili uwe bora lazima umfunge bingwa, ni nafasi ambayo tunayo kuhakikisha tunapambana kushinda.

“Wao wanataka ubingwa kwa sababu wanaongoza ligi na ndiyo matarajio yao, watakuwa wamejihamini na wanataka kila nafasi wafunge. Wanashambulia sana na wana uwezo mkubwa wa kukufungua. Kama timu tutacheza kwa tahadhari kubwa sana.

“Kiuhalisia lazima kwanza tuwaheshimu Yanga, tutacheza kwa transition, wakipoteza mpira tutashambulia kwa kushitukiza,” amesema Chamberi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live