Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kramo yupo nchini, hajaenda kwao - Ahmed Ally

Kramo Snsd Kramo yupo nchini, hajaenda kwao - Ahmed Ally

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: Voa

Nyota mpya wa Simba SC, Aubin Kramo yupo nchini na hajaenda kutibiwa nchini kwao kama ilivyoripotiwa awali.

Akizungumzia hali yake, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, alisema Kramo anaendelea na matibabu nchini.

"Aanaendelea na matibabu na kumekuwa na taarifa nyingi ooh ameruhusiwa kwenda kwao, Kramo yupo nchini anaendelea kutibiwa na madaktari wa Simba SC," alisema Ahmed Ally.

Kramo aliyesajiliwa dirisha kubwa lililopita, ameandamwa na majeraha na hajapata muda wa kucheza mechi yoyote ya kimashindano katika msimu mpya ulioanza.

Chanzo: Voa