Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kramo na mapenzi ya Mungu

Kramo Fiti(2) Aubin Kramo

Fri, 5 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika maisha Kuna mambo yanaweza kutokea wewe ni mabaya tofauti na ulivyo tarajia katika mipango yako hiyo ndiyo tunaitaga mipango ya Mungu Kuna mambo yanatokea bila wwe kupanga Yani haikuwa kwenye mipango yako Mungu anaweza kukupitisha kwenye majaribu wakati mwingine hili kukupa ukomavu au uthubutu katika jambo unalo fanya.

Mfano kwa nyota wa Simba kiungo Aubin Kramo ametoka inchini kwao Ivory coast katika klabu ya Asec Mimosa akiwa mchezaji tegemeo baada ya kufanya mambo makubwa katika ligi Simba wakavutiwa nae wakamsajili lakini baada ya kutua bongo kuanzia kwenye kipindi Cha pre Season Kramo akicheza mechi ya kirafiki utasikia amefunga lakini lazima ataumia na atakaa nje kidogo akirudi atafunga atakaa trna nje kiufupi aliandamwa na majeraha ambayo yamemfanya timu ya Simba kwenda kumfanyia vipimo baada ya kumfanyia vipimo na kugundua anatatizo la ligament katika goti lake na kufanyiwa upasuaji ulimuweka nje kwa kipindi Cha Mwezi mmoja.

Sasa mpango wa Mungu unakuwa unaonekana vipi kwa watu kama Hawa maana mpaka Sasa hivi mashabiki,Wanachama pamoja na Viongozi hawajua uwezo halisi wa kiungo huyu na timu Kwa kuwa ilifanya vibaya kuanzia November imechukua kocha Mpya Benchikha kidogo imeanza kurudi kwenye makali yake lakini pia katika dirisha hili imefanya maboresho kwahiyo unaweza kukuta maboresho haya ukichanganya na kocha Mpya na yeye Mungu akijalia kurudi kwenye kiwango Bora anaweza kuwa mfalme mpya ndani ya Simba Kramo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live