Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kramo bao hakijaeleweka Simba SC

Aubin Kramo Training Kramo bao hakijaeleweka Simba SC

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuelezwa kuwa taarifa yake ingetolewa jana, majibu ya vipimo vya nyota wa Simba SC, Aubin Kramo bado hayajatoka.

Akizungumza na Wasafi FM mapema hii leo Septemba 13, 2023 kuhusu maandalizi ya safari yao ya Zambia, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, alisema Kramo bado hakijaeleweka.

"Kuhusu nyota wetu Aubin Kramo, bado daktari wetu wa timu anasubiri majibu ya vipimo alivyochukuliwa hivyo yatakapotoka tutazungumza," alisema Ahmed.

Kuhusu safari yao ya Zambia kuwafata Power Dynamos mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Ahmed alisema timu itaondoka kesho.

"Kesho saa tano asubuhi ndio timu itaondoka. Leo ni zamu ya mashabiki, jumla ya mabasi matatu yataondoka kwa nyakati tofauti kuelekea Zambia," alisema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live