Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kramo afumua kikosi Simba

Kramo Simbaaaaaa Kramo afumua kikosi Simba

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba inaendelea kujifua mazoezini kabla ya kuanza safari kwenda Ndola Zambia kwa mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku wapya wa timu hiyo, Luis Miquissone na Aubin Kramo wakipangua kikosi kwa kumpa kocha Oliveira Roberto ‘Robertinho’ mfumo mpya kwa sasa.

Kramo amerejea kutoka kuwa majeruhi na ameanza kuwasha moto akiwa sambamba na Miquissone ambaye tangu arejee kikosini alionekana mzito, lakini kwa sasa yupo fiti na kumpagawisha Mbrazili huyo ambaye amekiri kwa sasa ana machaguo mengi atakayotumia kwenye mechi ya ugenini na nyingine zilizopo mbele yake.

Robertinho alisema kuwaka kwa wachezaji hao na kuibuka kwa vita ya namba kwa washambuliaji Moses Phiri, Willy Onana na Jean Baleke, kunamfanya sasa wajipange kwani kila mmoja ana nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, muhimu ni timu kupata matokeo mazuri uwanjani.

Robertinho amefunguka hayo baada ya kuwatumia mastaa hao kwenye mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Cosmopolitan na kushinda mabao 5-1 huku washambuliaji hao wakitupia kila mmoja bao moja moja.

Kocha huyo ambaye ni muumini wa kutumia mfumo wa 4-2-3-1, 4-1-3-2 na mara nyingine akitumia 4-1-3-1-1 aliliambia Mwanaspoti sasa atalazimika kubadili mfumo kutokana na aina ya mechi zilizo mbele yake huku akikiri kuwa wachezaji wake wapo katika nafasi nzuri ya kucheza.

Mfumo wa 4-2-3-1 amekuwa akitumia mabeki wanne, viungo wawili wa chini viungo washambuliaji wawili mmoja wa juu na mawinga wawili na wamekuwa wakitumika Clatous Chama, Said Ntibazonkiza na Kibu Denis na mshambuliaji mmoja ambaye ni Baleke au Phiri.

4-1-3-2 hapa anatumia mabeki wanne, kiungo mmoja mkabaji ambaye ni Sadio Kanoute au Fabrice Ngoma, Mzamiru Yassin, viungo washambuliaji watatu na washambuliaji wawili ambao ni chaguo lake mwenyewe kama alivyosema kuwa safu yake ya ushambuliaji ni imara.

Robertinho alisema kutokana na wachezaji kuanza kuongeza utimamu wa mwili tofauti na walivyoanza msimu huu, anaona kuna kila sababu ya kubadili mfumo wake wa uchezaji kulingana na mechi husika.

Aliongeza, ili mchezaji apate nafasi ya kucheza ni lazima amuonyeshe katika mazoezi yake kwa kuhakikisha anatimiza majukumu yote ya ndani ya uwanja atakayompa.

“Wachezaji wangu wote kwa asilimia kubwa nimewatumia kwenye mechi mbili za kirafiki tulizocheza wameonyesha wana kitu wanaweza kukifanya ndani ya timu mfano Aubin Kramo, Luis Miquissone wameonyesha kuimaraika zaidi.

“Kutokana na mabadiliko ya uchezaji wao wananifikirisha kuwa na mifumo tofauti na nilivyozoeleka na itakuwa inabadilika kutokana na mechi husika. Kuhusu ubora wa wachezaji kila mmoja amekuwa na umuhimu wake kulingana na mechi husika.” alisema kocha huyo aliyetua Januari mwaka huu kutoka Vipers ya Uganda.

Akizungumzia kutumia washambuliaji watatu kwenye mchezo mmoja ambao ni Onana, Phiri na Baleke alisema amegundua kitu kutoka kwao akiweka wazi kuwa akifanya hivyo ana uhakika wa kupata mfungaji bora kutoka katika nyota wake hao ambao amekiri kuwa kila mmoja anakuwa na kiu ya kufunga.

“Baleke, Onana na Phiri wote ni wachezaji wazuri kwenye umaliziaji na kila mmoja ana kiu ya kufunga hivyo naweza kutengeneza pacha nzuri na yenye faida kwa timu hasa kwenye suala la ushindani wa kupachika mabao mengi,” alisema Robertinho na kuongeza;

“Lakini wakati watatu hao wakifanya vizuri ameingia kati Kramo pia amekuwa mchezaji ambaye anajituma sana ameongeza chachu ya ushindani kwenye kikosi changu, nafurahia kuwa na wachezaji wenye malengo yanayofanana naamini sasa kila nitakayempa nafasi atanipa matokeo chanya.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: