Kiungo mpya wa Man City, Mateo Kovacic ametoa kauli ya kwanza kwa Chelsea baada ya kusajiliwa na Man City.
Kiungo huyo wa kati wa Croatia alifurahia kipindi cha mafanikio Stamford Bridge, akinyanyua mataji ya Uefa Champions League na Ligi ya Europa, lakini hakushinda tuzo yoyote ya ndani tangu kuwasili kwake akitokea Real Madrid.
Na sababu hiyo inaelezwa kumfanya Mateo Kovacic kujaribu bahati yake akiwa na jezi ya Manchester City.
“Nilifurahia msimu mzuri lakini sasa ni wakati wa kufungua ukurasa mpya na kushinda,” alisema Kovacic
“Man City ni klabu kubwa ambapo unaweza kushinda mengi na nitafanya kila niwezalo kujaribu kushinda kila mwaka. Kukusanya vikombe ndio jambo muhimu zaidi.”