Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kourt Zouma matatani

Kurt Zouma Beki wa Chelsea

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa klabu ya West Ham, Kurt Zouma anaweza kufunguliwa mashtaka baada ya kurekodiwa kwenye video akimpiga paka wake kama mpira.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 pia anaonekana kumpiga kofi usoni paka huyo, klabu yake imelaani kitendo hiko na kusema kuwa itashughulikia suala hilo.

Beki huyo anaonekana akimshambulia mnyama huyo kwenye jumba lake la kifahari kwa kumpiga teke kisha kumkimbiza mnyama huyo kuzunguka chumba chake cha kulia chakula mbele ya mtoto huku kaka yake akichukua video akicheka.

Katika 'clip' ya mwisho, anaonekana akimpiga paka kwa nguvu usoni.

Jana usiku, Zouma aliomba radhi kwa shambulio hilo na kusisitiza kuwa lilikuwa tukio la pekee. “Nataka kuomba msamaha kwa vitendo vyangu. Hakuna visingizio kwa tabia yangu, ambayo ninajuta kwa dhati"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live